Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul Bayt (as) -ABNA-, Utawala wa Kizayuni uliilenga Iran kwa mashambulizi yake ya kihasama na uchokozi siku ya Ijumaa na kuua kundi la makamanda wa kijeshi, wanasayansi wa nyuklia na raia wa kawaida.
Kuhusiana na hili, watu wapenda uhuru katika nchi mbalimbali (baadhi ya nchi), na watu mashuhuri wa kisiasa, kitamaduni, na watu wengine duniani kote walilaani uhalifu huo wa kikatili.
Dakta Hussein al-Mousavi, naibu mkurugenzi wa vyombo vya habari wa Harakati ya Nojaba amezungumza na ABNA na kulaani hujuma za utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran na kuuawa shahidi kundi la makamanda wa kijeshi, wanasayansi na watu wasio na hatia wa Iran na kuitaja hatua hiyo ya Israel kuwa ya woga.
Akizungumzia sababu za shambulio hilo la kikatili, Al-Moussawi alisema: "Kitendo hiki cha woga na cha kinyama, kilichofanywa na Israel na Marekani, ambacho kinasapoti na kuiunga mkono Israel, kilitokea ndani ya mfumo wa Marekani kushindwa kukabiliana na changamoto za kisiasa, migogoro ya kiuchumi, kijamii, ndani na nje, na jaribio lake la kusafirisha migogoro ya ndani nje ya nchi yake."
Aliendelea kusema: "Pia kushindwa kwa njia ya fedheha kwa sera ya Netanyahu ya kupata ushindi wowote katika vita dhidi ya Ghaza na kutokuwa na uwezo wa kusimamia migogoro ya ndani na jaribio lake la kukimbilia nje ya nchi ilikuwa sababu nyingine ya mashambulizi ya utawala huo dhidi ya Iran. Marekani na Israel zilijaribu kusalimisha Tehran na kuilazimisha kuachana na mpango wake wa amani wa nyuklia kwa kufanikisha mazungumzo chini ya moto."
Naibu afisa wa vyombo vya habari wa Harakati ya Nujaba alisema: "Kwa hiyo, uchokozi huu ni tishio kwa amani ya kimataifa na kitendo cha kiburi kwa upande wa Israel, ambayo inaendeleza mashambulizi yake ya kila siku, kuua, kuwafukuza na kuwasababishia njaa watu wa Gaza." Aliongeza: "Israel inapuuza maazimio yote ya Baraza la Usalama, Umoja wa Mataifa na maazimio mengine, na haizingatii maazimio yoyote ya kimataifa, na inapingana na maana zote za ubinadamu."
Al-Mousavi amesisitiza kuwa: "Tunaamini uwezo na nguvu za Jamhuri ya Kiislamu katika ngazi mbalimbali za kisiasa, kiuchumi, kijeshi na kiusalama, na tunajua kuwa taifa la Iran pamoja na uongozi wake wa busara na wa kimantiki unaunga mkono uwezo wa Jamhuri ya Kiislamu wa kupata ushindi katika mgogoro huu."
Akamalizia kwa kusema: "Vipengele hivi vya nguzu vitatosha kupata ushindi dhidi ya uvamizi wa Wazayuni na Wamarekani. Sisi katika Muqawama wa Kiislamu kwa ujumla, na hasa Harakati ya Nujaba, tunasimama upande wa Jamhuri ya Kiislamu katika kukabiliana na uchokozi huo."
Your Comment